WakalaOnlinePakua app

Mwanzo

Maswali ya mara kwa mara

Kila unachohitaji kujua kuhusu kutuma pesa kutoka Oman kwenda Tanzania na WakalaOnline. Hukupata jibu? Tuulize WhatsApp.

Kutuma pesa

Natuma pesa vipi?

Kwenye app bonyeza Tuma (au tuma ujumbe WhatsApp): namba ya simu au akaunti, jina la mpokeaji na kiasi (OMR). Mfano: 0712 345 678 Amina Juma 20. Utaona rate na TZS atakazopata. Bonyeza Weka oda — utaona kiasi na akaunti ya kulipa. Lipa, bonyeza ✅ Nimelipa na upakie picha ya risiti, na pesa inatumwa.

Naweza kutuma kwa mitandao gani?

Vodacom M-Pesa, Mixx by Yas, Airtel Money, HaloPesa na TTCL T-Pesa. Pesa inaingia moja kwa moja kwenye laini ya mpokeaji.

Naweza kutuma kwenye benki?

Ndiyo, benki zote kuu za Tanzania na Zanzibar — CRDB, NMB, NBC, PBZ, Equity, Exim, Stanbic na nyingine. Weka jina la benki, namba ya akaunti na jina la mwenye akaunti.

Pesa inachukua muda gani kufika?

Mara nyingi dakika chache baada ya malipo yako kuthibitishwa. Benki zinaweza kuchukua muda kidogo zaidi kulingana na benki.

Kiasi cha chini ni kiasi gani?

Unaweza kutuma kuanzia OMR 1.

Naweza kutuma kwa watu wengi kwa mara moja?

Ndiyo. Kwenye app ongeza wapokeaji wengi kwenye oda moja na ulipe malipo moja.

Nitamtumiaje tena mpokeaji wa zamani?

Wapokeaji wako wanahifadhiwa kwenye app. Nyumbani, chini ya “Tuma tena kwa”, bonyeza jina lake.

Rate na ada

Rate ya leo ni ngapi?

Rate ya sasa inaonyeshwa ukurasa wa mwanzo na kwenye app, au uliza WhatsApp — unajibiwa papo hapo.

Rate inabadilika lini?

Rate inasasishwa kulingana na soko. Rate unayoiona wakati unathibitisha oda ndiyo inayotumika.

Kuna rate maalum kwa kiasi kikubwa?

Ndiyo. Ukituma kiasi kikubwa unapata rate maalum, na inatumika yenyewe ukifika kiwango chake. Wateja wa kudumu wana rate yao.

Kuna ada ya kutuma?

Kama kuna ada kwa kiasi unachotuma, inaonyeshwa kabla hujalipa, pamoja na TZS kamili mpokeaji atakazopata. Hakuna gharama iliyofichwa.

Malipo na risiti

Nalipa vipi OMR?

Kwa benki au pesa ya simu hapa Oman. Ukiweka oda unaona kiasi na akaunti ya kulipa (bonyeza Nakili). Lipa, kisha bonyeza ✅ Nimelipa na upakie picha ya risiti. Rate ya oda inabaki kwa saa 2, baada ya hapo rate ya sasa inatumika. Unaweza pia kutuma risiti WhatsApp — inaunganishwa na oda yako.

Nimesahau kupakia risiti?

Fungua oda kwenye Nyumbani au Historia ya app na bonyeza ✅ Nimelipa (au 📎 Pakia risiti). Ulilipa mara mbili au tatu? Chagua risiti zote kwa pamoja (hadi 3), au bonyeza ➕ Ongeza risiti — iliyopo haifutwi. Unaweza pia kushiriki (share) picha ya risiti moja kwa moja kwenye app.

Nitajuaje pesa imefika?

Unaona hatua za oda wakati wowote — inasubiri, inatumwa, imefika. Pesa ikifika unapata taarifa na risiti ya wakala kwenye app au WhatsApp.

Naweza kupata risiti kama PDF?

Ndiyo. Fungua oda upakue risiti (PDF), na kwenye Historia unaweza kupakua taarifa ya miamala (PDF).

Salio na deni ni nini?

Ukilipa zaidi ya oda, ziada inakaa kama salio na unaweza kuitumia oda ijayo. Ukiwa na deni, unaliona Nyumbani kwenye app na unaweza kulilipa kwa risiti.

Makosa na kughairi

Nimekosea namba ya mpokeaji?

Wasiliana nasi mara moja WhatsApp ukiwa na Ref ya oda. Kama bado hujalipa, unaweza kughairi oda mwenyewe kwenye app.

Naweza kughairi oda?

Ndiyo, kama bado hujalipa — fungua oda na bonyeza Ghairi oda, au andika ghairi (na Ref ya oda) kwenye WhatsApp — inafutika papo hapo. Kama umeshalipa, kughairi au kurudishiwa pesa ni kupitia mazungumzo: fungua oda, bonyeza 💬 na tuandikie.

LUKU, bili na Nunua Rial

Naweza kulipia LUKU nikiwa Oman?

Ndiyo. Weka namba ya mita na kiasi; ukishalipa OMR, token inaonekana papo hapo kwenye oda yako (app au WhatsApp).

Bili gani nyingine mnalipa?

LUKU (TANESCO), TUKUZA, GePG, ZanMalipo, Maji, DStv, Azam TV na vocha.

Nunua Rial (TZS → OMR) ni nini?

Uko Tanzania au una mtu Tanzania? Weka oda kwenye app, lipa TZS kwa namba za wakala wetu, bonyeza ✅ Nimelipa na upakie risiti; wakala anahakiki, na OMR zinakufikia Oman kwa simu au benki.

App na WhatsApp

Napakuaje app ya WakalaOnline?

Android: bonyeza Pakua app na uisakinishe. iPhone: fungua wakalaonline.app/app kwenye Safari → Share → “Add to Home Screen”. App ni bure.

Kwa nini nipakue app?

Ukiwa na app unapata taarifa simuni pesa ikifika, wapokeaji wako wanahifadhiwa, unaona historia na risiti zote, unapakua taarifa ya miamala (PDF), na unaweza kuweka kufuli ya PIN.

Ninaingiaje kwenye app?

Kwa code inayotumwa WhatsApp — hakuna password ya kukumbuka.

Nikijibiwa na bot WhatsApp nifanye nini?

Hakiki maelezo aliyokuonyesha, kisha andika “ndiyo” kuthibitisha. Mhudumu yupo kwa maswali mengine.

Mnapatikana lini?

Tupo WhatsApp kila siku: +968 9723 2813.

Akaunti na usalama

Ninalindaje akaunti yangu?

Kwenye app: Akaunti → Usalama. Washa Kufuli ya app (PIN) na alama ya kidole / uso, ficha salio, au “Toka kwenye simu zote” ukipoteza simu.

“Mlete rafiki” inafanyaje kazi?

Kila mteja ana code yake. Rafiki akitumia code yako, nyote mnapata zawadi ya TZS.

Nitajuaje naongea na WakalaOnline halisi?

WhatsApp yetu ni +968 9723 2813 na tovuti ni wakalaonline.app pekee. Hatutakuomba kamwe PIN, OTP au code yako ya kuingia.

WakalaOnline ni huduma ya nani?

WakalaOnline ni huduma ya FastConnect Agency Limited, yenye ofisi Muscat, Oman na Zanzibar, Tanzania.

Tuma pesa sasaTuulize WhatsApp