Oman → Tanzania

Tuma pesa nyumbani, kwa sekunde.

Rate nzuri, risiti papo hapo, na unafuatilia kila order mpaka ifike Tanzania. Kwa simu, benki, LUKU na bili.

Huduma ya FastConnect Agency Limited · Kiasi cha chini OMR 1

Rate ya sasa Inapakia…

1 OMR =

— — —TZS

Rate ya leo haikupatikana kwa sasa. Uliza kwa WhatsApp — unajibiwa papo hapo.

Muscat · OMRTanzania · TZS

Jinsi inavyofanya kazi

Hatua tatu, na pesa inafika.

Hakuna fomu ndefu. Unatuma maelezo kwa ujumbe mmoja, unalipa OMR hapa Oman, na mpokeaji anapata TZS kwenye simu au akaunti yake.

Tuma maelezo ya mpokeaji

Kwa WhatsApp au kwenye app: namba ya simu au akaunti, jina la mpokeaji, na kiasi (OMR). Mfano: 0712 345 678 Amina Juma 20.

Hakiki na ulipe OMR

Tunakuonyesha rate, TZS atakazopata na maelezo ya kulipia. Unalipa kwa benki au simu hapa Oman na kutuma picha ya risiti.

Pesa inafika, risiti inakuja

Wakala wetu Tanzania analipa, na unapata risiti ya malipo kwenye WhatsApp au app yako. Kwa LUKU, token inaonekana papo hapo.

Unatuma wapi?

Simu, benki, au bili — kila kona ya Tanzania.

Pesa ya simu

Inaingia moja kwa moja kwenye laini ya mpokeaji.

  • Vodacom M-Pesa
  • Mixx by Yas
  • Airtel Money
  • HaloPesa
  • TTCL T-Pesa

Akaunti ya benki

Kwa akaunti za benki zote kuu za Tanzania na Zanzibar.

  • CRDB
  • NMB
  • NBC
  • PBZ
  • Equity
  • Exim
  • Stanbic
  • na nyingine

LUKU na bili

Lipa moja kwa moja kutoka Oman, na token au uthibitisho unakuja kwako.

  • LUKU (TANESCO)
  • TUKUZA
  • GePG
  • ZanMalipo
  • Maji
  • DStv
  • Azam TV
  • Vocha

Kwa nini WakalaOnline

Unajua pesa yako iko wapi, kila wakati.

Risiti kwa kila order

Risiti ya wakala inakuja kama picha kwenye WhatsApp au app. Unaweza kuipakua kama PDF.

Fuatilia hatua kwa hatua

Inasubiri, inatumwa, imefika. Unaona hali ya order yako wakati wowote, bila kuuliza.

Rate bora kwa kiasi kikubwa

Ukituma kiasi kikubwa unapata rate maalum. Wateja wa kudumu wana rate yao.

Mlete rafiki, mfaidike wote

Kila mteja ana code yake. Rafiki akitumia code yako, nyote mnapata bonus ya TZS.

Hesabu

Mpokeaji atapata kiasi gani?

Weka OMR unazotuma. Hesabu inatumia rate ya sasa; rate ya kiasi kikubwa inatumika yenyewe ukifika kiwango chake.

Mpokeaji atapata—

Rate inapakia…

Tuma kiasi hiki kwa WhatsApp

App ya WakalaOnline (Android)

Tuma, fuatilia, na upate risiti — yote kwenye app moja.

Unaingia kwa code ya WhatsApp. Hakuna password ya kukumbuka.

  • Rate ya leo na hesabu ya TZS papo hapo
  • Wapokeaji wako wanahifadhiwa; tuma tena kwa kubonyeza mara moja
  • Tuma kwa wapokeaji wengi kwa malipo moja
  • Taarifa kwenye simu pesa ikifika, na taarifa ya miamala ya mwezi (PDF)

Android pekee kwa sasa. Baada ya kupakua, fungua faili na uruhusu "Install from this source".

Mawasiliano

Tupo WhatsApp kila siku.

WhatsApp ya biashara

+968 9723 2813

Tuma ujumbe mmoja wenye namba, jina na kiasi. Ukijibiwa na bot, andika "ndiyo" kuthibitisha; mhudumu yupo kwa maswali mengine.

Fungua WhatsApp

Maswali ya mara kwa mara

Pesa inachukua muda gani kufika?

Mara nyingi dakika chache baada ya malipo yako kuthibitishwa. Order za benki zinaweza kuchukua muda kidogo zaidi kulingana na benki.

Nalipa vipi OMR?

Kwa benki au pesa ya simu hapa Oman. Maelezo ya akaunti unapewa baada ya kuthibitisha order, kisha unatuma picha ya risiti.

Nikikosea namba ya mpokeaji?

Wasiliana nasi mara moja kwa WhatsApp ukiwa na Ref ya order. Kabla malipo hayajathibitishwa, unaweza kughairi order kwenye app.

Rate inabadilika lini?

Rate inasasishwa kulingana na soko. Rate unayoiona wakati unathibitisha order ndiyo inayotumika.